Yanga imethibitisha kuwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi, Februari 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, utachezwa kuanzia saa moja usiku
Ratiba iliyotolewa na Azam TV ambao wataonyesha mchezo huo mbashara, ilikuwa ikionyesha muda wa mchezo ni saa mbili na nusu usiku
Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa muda wa mchezo ni saa moja usiku akiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu

ADVERTISE HERE