Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City yanaendelea wakiwa na malengo ya kushinda mchezo huo
Wakiwa na dhamira ya kutwaa ubingwa msimu huu, Manara amesema kila mchezo kwao ni fainali na hawatizami matokeo ya michezo iliyopita
"Sisi tunaangalia kesho yetu, matokeo ya nyuma yamepita. Tunajua tunaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 10 lakini sisi hilo hatufikirii. Tunachoangalia ni kuweza kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Mbeya City na baada ya hapo tunamuangalia mpinzani anayefuata"
"Wachezaji wetu wanafahamu uhitaji wa ubingwa msimu huu, wataendelea kupambana kuhakikisha wanakamilisha lengo hilo," alisema Manara katika mahojiano na Azam TV
Manara amesema Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 10 huku timu zote zikiwa na michezo sawa. Jambo hilo halikutokea katika misimu yote minne iliyopita ambayo Simba ilitwaa ubingwa