Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Abdulrazak amesajiliwa na klabu ya RS Berkane kwa mkopo akitokea klabu ya Khouribga aliyojiunga nayo baada ya kuachwa na Yanga
Fiston alisajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita, akitokea ENPPI ya Misri
Katika miezi sita aliyoitumikia Yanga, Fiston alifunga bao moja tu kwenye ligi. Hakuweza kuwashawishi mashabiki na hata benchi la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi
Lakini amekuwa na kiwang bora tangu alipotua Morocco akiifungia Khouribga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo sita
Amejiunga na Berkane ambayo pia ilimsajili winga wa zamani wa Yanga Tuisila Kisinda
ADVERTISE HERE