Nyota wa Yanga Yannick Bangala na Djuma Shabani leo wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Bahrain
Wachezaji hao wanatarajia kurejea nchini baada ya mchezo huo wa maandalizi kwa ajili ya mchezo wa play-off kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Morocco
Yanga itamuhitaji Bangala Jumamosi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Djuma ataendelea kukosekana akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu
Tayari amekosa mchezo mmoja wa kombe la FA uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Mbao Fc
Kiungo Mukoko Tonombe aliyesajiliwa na TP Mazembe hivi karibuni, ni miongoni mwa wachezaji katika kikosi cha DR Congo

ADVERTISE HERE