Baada ya kukosekana kikosini kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha aliyopata kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, kiungo fundi Feisal Salum 'Fei Toto' amepona majeraha akiwa sehemu ya kikosi kinachojiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa Jumamosi, Februari 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kurejea kwa Feisal ni habari njema kwa kocha Nasreddine Nabi ambaye timu yake ilikosa huduma ya mchezaji huyo katika michezo miwili iliyopita
Mbeya City wanaoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya NBCΒ tayari wako jijini Dar es salaam
Leo walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya DTB uwanja wa Chamazi mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Nabi alipata nafasi ya kwenda Chamazi kushuhudia mchezo huo
ADVERTISE HERE