Mabeki Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu 'Ninja' tayari wamerejea nchini baada ya kutibiwa majeraha yao Tunisia
Wachezaji hao tayari wameanza mazoezi mepesi na pengine wanaweza kurejea uwanjani karibuni

Hii ni habari njema kwa Yanga hasa kurejea kwa Kibwana ambaye amekuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi
Aidha mshambuliaji Yacouba Songne nae anaendelea na program maalum ya mazoezi kukiwa na matumaini kuwa nae anaweza kurejea uwanjani mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa
Yacouba alifanyiwa upasuaji mkubwa wa goti na alitarajia kukaa nje mpaka mwezi May
ADVERTISE HERE