Baada ya kuwasili jijini Mwanza mapema leo, jioni kikosi cha Yanga kikaanza maandalizi yake kuelekea mchezo wa raundi ya nne kombe la FA dhidi ya Mbao Fc
Yanga imefanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja wa CCM Kirumba huku uongozi ukizuia mashabiki kuingia kushuhudia mazoezi hayo
Idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza kushuhudia mazoezi ya mabingwa hao wa kihistoria
Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kutua jijini Mwanza msimu huu, ni wazi mashabiki wana shauku kubwa ya kuwaona wachezaji wao
Yanga itakamilisha maandalizi yake ya mwisho katika uwanja huo siku ya kesho tayari kwa mtanange utakaopigwa Jumamosi
ADVERTISE HERE