Yanga imefanikiwa kuilaza Ruvu Shooting kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 14, uliopigwa kwenye dimba la Taifa.
Bao pekee la Yanga liliwekwa kimiani na winga Pius Buswita aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahim Ajib kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza.
Licha ya kumiliki mpira kwenye kipindi cha kwanza, Yanga haikutengeneza nafasi nyingi.

Kinda Yohana Nkomola aliyepata nafasi ya kuanza leo, alishindwa kumaliza kipindi cha kwanza baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Emanuel Martin.
Katika kipindi cha pili ni Ruvu Shooting iliyotawala zaidi na kama si uzembe wa washambuliaji wake, wangeweza kusawazisha bao na pengine kufunga mabao zaidi.
Juma Mahadhi aliyeingia kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe kwenye dakika ya 68, alikosa bao la wazi dakika za majeruhi baada ya kushindwa kuunganisha krosi ya Emanuel Martin.

Aidha mlinzi wa pembeni Hassani Kessy alifanya kazi ya ziada mara kadhaa kusahihisha makosa yaliyokuwa yakifanywa na walinzi wa kati Andrew Vicent na Said Juma.
Ukiacha matukio ya hapa na pale, kipindi cha pili wanajeshi wa Ruvu Shooting walicheza mpira wa 'kibabe' zaidi uliopelekea vijana wa Yanga kujibu mapigo na kusababisha mchezo huo utawaliwe na rafu nyingi.
Ushindi ndio matukio yaliyohitajiwa na Yanga. Sasa imefikisha alama 25 na kuchupa hadi nafasi ya tatu.
Katika michezo mingine, Azam FC imeilaza Prisons mabao 2-0 na kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi huku Mwadui FC ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda FC.
Mchezo unaofuata, wiki ijayo Yanga itakuwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi kuivaa Azam FC .

ADVERTISE HERE