Baada ya mapumziko ya siku ya moja, kikosi cha Yanga kimerejea kambini kujiandaa na mchezo wa raundi ya nne kombe la FA dhidi ya Mbao Fc ambao sasa umehamishiwa uwanja wa CCM Kirumba
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Januari 29 ukihamishwa kutoka dimba la Benjamin Mkapa kutokana na uwanja huo kuwa na matumizi mengine siku ya Jumamosi
Ni uamuzi wa kiungwana uliofanywa wa viongozi wa Yanga kuwapelekea Wananchi wa Mwanza burudani kwa mara ya kwanza msimu huu
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kutinga hatua ya 16 bora katika michuano hiyo ambayo Wananchi wanautaka ubingwa
Β
ADVERTISE HERE