Chico yuko tayari kuwakabili Polisi Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2022
Chico yuko tayari kuwakabili Polisi Tanzania

Winga mpya wa Yanga Chico Ushindi anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid baadae leo

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni Fc akicheza dakika chache, leo anaweza kupata dakika nyingi zaidi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi katika Mkutano na Wanahabari jana, alisema atatumia mazoezi ya mwisho jana jioni kuona kama anaweza kumtumia winga huyo leo au la

Chico yuko timamu kiafya na alifanya mazoezi ya mwisho kikamilifu na wenzake

Kuna wasiwasi juu utimamu wa kiungo Feisal Salim ambaye alipata majeraha mazoezini, kama hatakuwa sehemu ya kikosi leo, ni wazi Chico anaweza kuwa na nafasi ya kuanza huku Saido akisogea kati nafasi ya Feisal

Chico ametua Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea klabu ya TP Mazembe, na alikuwa na mwanzo mzuri katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni Fc

Katika mchezo huo alisababisha mkwaju wa penati uliopelekea bao la pili la Yanga, kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’