Hii hapa sababu ya Kanku kukosekana kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2018
Hii hapa sababu ya Kanku kukosekana kikosini
Beki mpya wa Yanga, Mkongo Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ameshindwa kujiunga na timu tangu asajiliwe Desemba kutokana na matatizo ya kifamilia.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika katika mahojiano maalum na mtandao wa Bin Zubeiry.

Nyika amesema kwamba Kanku tayari ni mchezaji wa Yanga na atajiunga na timu mara atakapomaliza matatizo yake ya kifamilia.

"Kanku ana matatizo ya kifamilia na ni makubwa ndiyo maana tumemruhusu kwa sasa aende kuyashughulikia, akimaliza atakuja kuanza kazi, na muda upo, Ligi bado mbichi sana,Ò€amesema Nyika.

Lakini pia, Nyika amesema kwamba uhamisho wake wa kimataifa (ITC) nao pia ulikuwa unasumbua ila kwa sasa wapo kwenye hatua za mwisho kuupata.

Baada ya kuwa majaribio tangu Agosti, Kanku alisaini mkataba wa miaka miwili Desemba mwaka jana na kuzima kabisa uwezekano wa beki Mtogo, Vincent Bossou kurejeshwa Jangwani, licha ya kupigiwa debe na wadau mbalimbali wa klabu hiyo, arejeshwe kikosini.

Bossou alimaliza mkataba wake msimu uliopita baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka miwili alitarajiwa kuendelea kutokana na kufanya vizuri, lakini klabu haikumpa mkataba mpya baada ya mazungumzo ya muda mrefu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’