Uongozi wa timu ya soka ya Polisi Tanzania Fc umethibitisha kupeleka mchezo dhidi ya Yanga SC katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Ni baada ya uwanja wa Ushirika uliopo mjini Moshi kuwa na matumizi mengine
Mchezo huo ulipangwa kupigwa Jumapili katika uwanja wa Ushirika lakini siku moja kabla ya mchezo yani Jumamosi kutakuwa na tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
Yanga tayari iko mkoani Arusha ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo ambapo jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbuni Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
ADVERTISE HERE