Kwa Yanga hii waandike maumivu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jan 2022
Kwa Yanga hii waandike maumivu

Ukiangalia mwenendo wa ligi kuu ya NBC, Yanga wako kileleni mwa msimamo wa ligi kwa miezi kadhaa sasa wakiongoza kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Simba wana mchezo mmoja wa kiporo ambao hata kama watashinda watakuwa na deni la alama tano kuweza kuifikia Yanga hapo juu

Katika msimu uliopita pia Yanga iliongoza ligi kwa muda mrefu lakini hawakuweza kuendeleza kasi hiyo mpaka mwisho na Simba kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Akihojiwa na Wasafi FM katika kipindi cha michezo jana, Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally alitumia kilichotokea msimu uliopita kuwapa imani mashabiki wa Simba kuwa hata msimu huu mambo yatakuwa vilevile

"Sisi muda wetu wa kuongoza ligi bado haujafika. Ni kawaida yao wanaongoza ikifika wakati flani wanakata upepo na hapo sisi tunachukua nafasi yetu hadi ubingwa," alisema Ahmed

Hata hivyo Msemaji wa Yanga Haji Manara amejibu kauli hiyo akibainisha kuwa maisha ya kukariri hayana nafasi kwani msimu huu ni tofauti kabisa na msimu uliopita

Manara amesema licha ya kuwa wamejipanga kwelikweli kuhakikisha yaliyotolea msimu uliopita hayajirudii, lakini pia wana kikosi bora zaidi kuliko timu yoyote

"Hao wanajitoa ufahamu lakini Yanga ndio timu bora mara dufu kuliko wao kwa takwimu zote. Sisi tumejipanga na jambo uzuri tunafahamu njia zao za 'shupli' na mbinu ambazo wamekuwa wakitumia"

"Soka sio mchezo wa kukariri kuwa jana ni leo na leo ni kesho, dakika 90 ndizo zinazoamua mshindi," alitamba Manara

Msimu huu Yanga inajivunia safu bora ya ushambuliaji ambapo kwa mujibu wa takwimu Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi kuliko timu nyingine lakini pia ndio timu iliyoruhusu mabao machache

Fiston Mayele ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mabao sita akifuatiwa kwa karibu na Feisal Salum (4), Saido Ntibazonikza (4) na Jesus Moloko (3)

Changamoto ya Yanga msimu uliopita ilikuwa kwenye safu ya ushambuliaji kwani timu ilikuwa haifungi idadi ya mabao ya kutosha na kupelekea michezo mingi kumalizika kwa sare

Msimu huu Yanga imefunga wastani wa mabao mawili katika kila mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
59m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’