Kikosi cha Yanga kinashuka kwenye dimba la Taifa kesho Jumapili, Januari 21 kuivaa Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 14.
Yanga haijapata ushindi kwenye michezo mitatu iliyopita na kujikuta ikiachwa kwa pointi saba na vinara wa ligi Simba.
Hali hiyo inaufanya mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting uwe ni lazima kwa Yanga kupata ushindi ili kuendelea kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wake.
Matokeo tofauti na ushindi si kwamba yatafifisha ndoto ya kutetea ubingwa tu, pia huenda yakashusha kabisa morali ya wachezaji na mashabiki.
Hali hiyo itahatarisha zaidi mustakabali wa Yanga ambayo inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Azam FC wiki ijayo kwenye dimba la Chamazi.
Yanga imekuwa ikijifua kwa nguvu kwenye dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE