Winga mpya wa Yanga Chico Ushindi ameeleza furaha yake baada ya usajili wake kukamilishwa kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa juzi Januari 15 2022
Ushindi ametua Yanga akitokea klabu ya TP Mazembe akisaini mkataba wa miaka miwili
Ni pendekezo la kocha Nasreddine Nabi ambaye alihitaji winga mwenye kasi kuziba nafasi ya Yacouba Songne ambaye atarejea uwanjani msimu ujao
"Kocha (Nabi) alinipigia simu nikiwa bado Congo na akaniambia kitu gani anataka nifanye hapa Yanga nimefurahia mazungumzo yangu na kocha"
"Sina wasiwasi na uwezo wangu wala hicho anachotaka nifanye jambo zuri nakuja kwenye timu yenye wachezaji wakubwa waliokomaa kiakili"
"Mimi nafurahi nikicheza kushambulia kutoka pembeni. Naweza kufunga na zaidi kutengeneza nafasi wenzangu wengine wafunge tukicheza kwa ushirikiano mambo yatakuwa rahisi," alisema Ushindi