Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa kiungo Mukoko Tonombe atajiunga na TP Mazembe baada ya klabu kufikia makubaliano
Bumbuli ametoa ufafanuzi kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya Yanga kumsajili Chico Ushindi na TP Mazembe kumsajili Mukoko, kila klabu imefanya usajili kulingana na mahitaji yake
"Kuna jambo halizungumzwi sawa, sisi tulimtaka Chico Ushindi kulingana na mahitaji yetu na wao TP Mazembe wakamtaka Mukoko kulingana na mahitaji yeo. Sasa kwa kuwa sisi tunao viungo wengi na Mukoko amebakisha miezi sita tu katika mkataba wake tukaona tunaweza kumruhusu akajiunge na Mazembe"
"Hatujabadilishana wachezaji, Yanga imesajili kulingana na mahitaji yake na hivyo hivyo kwa TP Mazembe," alisema Bumbuli
Mukoko hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichokuwa mkoani Tanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union akibaki jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili wake kwenda TP Mazembe
Wananchi wataendelea kuthamini mchango wake katika klabu ya Yanga, mmoja wa wachezaji walioonyesha mapenzi makubwa kwa klabu hii yenye historia kubwa
Presha imekuwa kubwa kwake msimu huu baada ya kukosa uhakika wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza
Mukoko ni mchezaji mzuri ambaye anahitaji kucheza kila siku lakini imekuwa ngumu kwake kupata nafasi ya kudumu mbele ya Khalid Aucho na Yannick Bangala ambao wako katika kiwango bora zaidi yake