Kwa hakika wakati mwingine umri ni namba tu, mkongwe Saido Ntibazonkiza ameendelea kulidhihirisha hilo
Kwa mara nyingine leo Saido ameibeba Yanga kule mkoani Tanga katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union
Bao la kwanza lilianzia katika mguu wake na pia akaweka kambani bao la pili kwenye dakika za majeruhi
Lilikuwa ni bao lake la nne msimu huu akiendelea kuwa chachu ya ushindi wa Yanga kila anaokuwa uwanjani
Chini ya profesa Nabi Saido amekuwa mpambanaji, kila wakati anahusika katika kuhakikisha Yanga inapata matokeo
ADVERTISE HERE