Wananchi wako mkoani Tanga ambapo jioni ya leo watashuka katika uwanja wa Mkwakwani kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Msimu huu Yanga imedhamiria kutwaa ubingwa, ili kufanikisha hilo lazima kushinda kila mchezo unaokuja mbele
Uwanja wa Mkwakwani umekuwa mgumu kutoa matokeo kwa Yanga katika kipindi cha miaka saba iliyopita
Hivyo leo Wananchi wamedhamiria kubadili historia hiyo kwa kuibuka na ushindi na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara amesema sio mchezo wa kisasi kwao lakini ni mchezo ambao wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu ili kutimiza malengo yao
Coastal Union ni moja ya timu bora msimu huu hivyo ni mchezo ambao mashabiki wa soka jijini Tanga watakaokwenda uwanjani na wale watakaofuatilia kupitia Azam TV, watapata burudani
Ni saa kumi kamili jioni katika uwanja wa Mkwakwani