Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema kesho Jumamosi kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa watamambulisha mchezaji mpya wa kigeni aliyesajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria
Mapema leo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa alisema walikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa nyota wa Kimataifa, usajili ambao utatikisa nchi
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jijini Tanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Jumapili, Januari 16 katika uwanja wa Mkwakwani, Manara alisema jina la mchezaji huyo na nchi anayotoka itafahamika kabla ya dirisha la usajili kufungwa hapo kesho
"Kabla dirisha hakijafungwa kesho, Tutamtangaza mchezaji wa kimataifa , anacheza nafasi gani? Anatoka nchi gani? Naomba tusubiri kesho," alisema Manara
Akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union, Manara amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanaondoka Tanga na alama zote tatu
"Tunajua Coastal ni hodari sana kwenye siasa za mpira hasa hasa nje ya uwanja. Tunajua wana mbinu nyingi sana lakini tumejipanga"