Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Jumapili, Januari 16 katika uwanja wa Mkwakwani
Bumbuli amesema wanafahamu misimu michache nyuma imekuwa sio rahisi kwao kupata ushindi mkoani Tanga, lakini hiyo ni historia tu. Amewataka Coastal Union wasiishi kwa mazoea kwani timu wanayokwenda kukutana nayo sio ya msimu uliopita
"Tumejipanga vizuri kupambana na Coastal Union, wasitegemee yaliyotokea mwaka jana yatatokea tena mwaka huu"
"Msimu huu tumekuja kivingine, tuna utaratibu mpya ambao tunakwenda nao lakini pia tuna timu mpya. Tunawatahadharisha tu, kuti la mazoea ndio humuangusha mkwezi," alitamba Bumbuli
ADVERTISE HERE