Dirisha dogo la usajili ambalo lilifunguliwa Disemba 16 2021, linatarajiwa kufungwa Jumamosi, Januari 15 2022
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 'TFF' limezitaka klabu kuhakikisha zinakamilisha michakato yote ya usajili ndani ya muda ikiwa ni pamoja na uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi
Taarifa iliyotolewa na TFF imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza pale dirisha litakapofungwa
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajiliwa wachezaji wanne katika dirisha hili, Salum Abubakar, Denis Nkane, Abdultwalib Mshery na Crispine Ngushi
Hakuna usajili wa nyota wa kigeni uliofanyika mpaka sasa ingawa zipo tetesi kuwa huenda kukawa na 'suprise' ndani ya saa 48 zilizobakia
ADVERTISE HERE