Winga mpya wa Yanga Denis Nkane alikosa mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi hapo jana dhidi ya Azam Fc kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya KMKM
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Nkane anaendelea na matibabu akiwa na uvimbe juu ya goti lakini anatarajiwa kurejea uwanjani mapema
Jana Yanga pia ilimkosa kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' ambaye aligua malaria visiwani Zanzibar
Katika mchezo dhidi ya Azam Fc, kiungo Feisal Salum akapata majeraha, huku Zawadi Mauya akilazimika kutibiwa kwa dakika kadhaa kabla ya kurejea uwanjani baada ya kuchezewa rafu mbaya na Frank Domayo
Moja ya sababu iliyopelekea viongozi wa Yanga kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kushiriki michuano hiyo ni pamoja na kuwaepusha na changamoto hii ya majeraha