Kocha wa makipa klabu ya Yanga Razak Siwa amesema wako tayari kuikabili Azam Fc kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi ambao utapigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Amaan, saa kumi na robo jioni
Siwa amesema dhamira yao ni kuhakikisha wanatetea ubingwa wa michuano hiyo walioshinda mwaka jana na kuwa hawana hofu yoyote kuelekea mchezo huo
"Tuko tayari kucheza na Azam Fc, maandalizi yanakwenda vizuri na hatuna wasiwasi wowote"
"Kuna wachezaji walikosekana kwenye mchezo wa kwanza, wengine wakaonekana kwenye mchezo wa pili hivyo tutarajie wengine kuonekana kwenye mchezo huo wa nusu fainali"
"Tunakwenda kwenye mchezo huo tukiwa na lengo moja tu, kushinda, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji kushinda ili tuweze kuingia fainali," alisema Siwa