Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mwadui FC juzi, Yanga inajifua kwenye dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting.
Matokeo ya mchezo uliyopita hayakulifurahisha benchi la ufundi na sasa wamepania kufanya masahihisho ya makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting.
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema ni mapema sana kuiondoa Yanga kwenye mbio za ubingwa hasa ikizingatiwa hata mzunguuko wa kwanza bado haujakamilika.
Habari njema ni kurejea kwenye benchi la Ufundi kwa kocha Mkuu George Lwandamina ambaye alikosekana kwenye michezo kadhaa kutokana na kibali chake cha kufanya kazi nchini kuisha muda wake.

ADVERTISE HERE