Mambo muhimu baada ya Katiba Mpya kuanza kutumika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2022
Mambo muhimu baada ya Katiba Mpya kuanza kutumika

Baada ya kusajiliwa kwa Katiba ya Yanga, katiba imeanza kutumika rasmi tarehe 01/01/2022

Hatua inayofata ni kuhakiki Wanachama wa Yanga nchi nzima. Wanachama wa Yanga ni lazima wahuishe uanachama wao kwenye mfumo wa kidigitali.

Wanachama wakisha hakikiwa, Matawi yote nchini ni lazima yafanye uchaguzi ili waweke muundo wa Uongozi kwa mujibu wa katiba mpya, ambao ni tofauti na ulivokua zamani. -

Kupitia matawi tutapata wawakilishi wa kila tawi kwenye mkutano mkuu, tofauti kama ilivyokua mwanzo ambapo kila mwanachama alikua mjumbe wa mkutano mkuu.

Baada ya Uchaguzi wa Matawi na kuweza kuwapata Wawakilishi wa Mkutano mkuu, tutaenda kwenye Uchaguzi Mkuu

Kwenye Uchaguzi Mkuu tunaenda kumpata Rais, Makamu wa Rais, na wajumbea watano watakao chaguliwa na Mkutano Mkuu

Ni vyema WanaYanga kujipatia nakala yako ya Katiba, kuisoma na kuielewa juu ya Muundo mpya wa Uongozi kwa mujibu wa Katiba mpya na kutumia fursa hii

Yanga ni ya Wanachama, na kuwa Mwanachama lazima ulipe ada yako ya Uanachama

Kwa hisani ya Mkurugenzi wa Sheria Yanga, Simon Patrick

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’