Licha ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMKM, Yanga imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuongoza kundi B
Heritier Makambo aliitanguliza Yanga kwa bao safi kwenye kipindi cha kwanza akimalizia krosi ya Dickson Ambundo
KMKM wakarejea mchezoni kwa kusawazisha bao hilo kabla ya Feisal Salum kufunga bao la pili ambalo lilionekana kama limeihakikishia Yanga ushindi kabla ya KMKM kusawazisha tena kwenye dakika za lala salama wakitumia makosa ya wachezaji wa Yanga waliozembea kuzuia mpira wa adhabu uliopigwa haraka
Yanga ilihitaji alama moja tu kusonga mbele huku KMKM wakihitaji ushindi lakini ni Yanga iliyofanikiwa kutinga nusu fainali
ADVERTISE HERE