Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumamosi kutoka Ubelgiji alikokwenda kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya kifamilia
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Nabi aliomba siku tano na kama hakutakuwa changamoto yoyote katika usafiri, atarejea nchini kesho na moja kwa moja kuelekea visiwani Zanzibar
"Kocha wetu alipata matatizo hivyo akaomba siku tano kurejea kwao kuyashughulikia. Kama hakutakuwa na changamoto ya usafiri atarejea nchini January 08 na tutarajie kumuona kwenye michezo ijayo kuanzia hatua ya nusu fainali," alisema Bumbuli
Hata hivyo Bumbuli amesema kukosekana kwa Nabi sio tatizo kwani aliacha program zote za mazoezi kwa Kocha Msaidizi, Cedric Kaze
"Sisi tuna makocha wenye vigezo vyote. Kocha Msaidizi anaweza kuiongoza timu msimu mzima na hata kocha mkuu anaweza kuiongoza timu bila ya kocha msaidizi"
"Hawa ni makocha ambao CV zao zimekamilika, hatuhitaji kuleta mtu mwingine kuwashikia eti kwa kukosa vigezo," alitamba Bumbuli