Usajili wake ulikamilishwa juzi usiku, jana mchana akapanda boti kuelekea visiwani Zanzibar na usiku akashuka uwanja wa Amaan kuikabili Taifa ya Jan'gombe katika michuano ya kombe la Mapinduzi
Crispine Ngushi, alipata nafasi ya kucheza mchezo huo ingawa hakuanza katika kikosi cha kwanza
Ngushi ameonyesha ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa kwani pamoja na kutofanya mazoezi na wenzake, alionekana kuelewa kwa haraka majukumu yake na nini anapaswa kufanya
Wananchi watamfurahia zaidi baadae atakapokuwa amepata muda wa kufanya mazoezi na wenzake
Wenzake Abdultwalib Mshery, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Denis Nkane walipata siku chache za kufanya mazoezi na wenzao kabla ya kujumuishwa kwenye kikosi
ADVERTISE HERE