Jana usiku Yanga ilicheza mchezo wa kwanza wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya Jang'ombe na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0
Heritier Makambo ambaye alikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa, alifunga 'bao la kideo' huku Denis Nkane akianza vyema maisha yake kwa Wananchi akifunga bao la pli
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi baada ya wachezaji kadhaa kukosekana kutokana na sababu mbalimbali
Pamoja na mabadiliko hayo, Yanga ilikuwa katika ubora uleule, hii ni habari mbaya kwa timu pinzani kwani Wananchi wameamua kumaliza unyonge 'kibabe'
Hicho kikosi kilichokwenda Visiwani Zanzibar kinao uwezo wa kutetea taji la Mapinduzi kwa msimu wa pili mfululizo
Katika mchezo wa jana, Kaze alianza na Mshery, Boxer, Bryson, Mwamnyeto, Yassin, Mauya, Nkane, Sureboy, Ambundo, Kaseke na Makambo
Waliokuwa nje ni Johora, Job, Msenda, Balama, Ali Said na usajili mpya Crispine Ngushi
Wachezaji ambao hawakuwepo kabisa kutokana na sababu mbalimbali ni Djigui Diarra, Djuma Shabani, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yannick Bangala, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Fiston Mayele, Saido Ntibazonkiza na Jesus Moloko
Sasa angalia kule upande wa pili kama wanaweza kubadili timu yao kwa kiwango hiki!