Makambo, Nkane waizamisha Taifa Jan'gombe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jan 2022
Makambo, Nkane waizamisha Taifa Jan'gombe

Ikiwatumia nyota wao wapya waliowasajili Denis Nkane pamoja na staa wa Haritier Makambo. Yanga wameonyesha ubora wao kuwa hawabahatishi na kuifunga Taifa ya Jang'ome  mabao 2-0.

Yanga wamecheza na Taifa Jang'ombe ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi mashindano yanayoendelea Uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.

Makambo ndiye alianza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya 32 akipiga shuti la mbali lililomshinda kipa wa Taifa Jang'ombe Hussein Abel. Wakati Makambo akifunga bao hilo Denis Nkane alitikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya 49 huku akikosa bao lingine dakika ya 56 ambapo shuti lake lilitoka nje ya goli.

Nkane aliyesajiliwa akitokea Biashara United ameonekana kuwa bora wakati wote wa mchezo huo huku akisumbua ngome ya wapinzani wao.

Taifa Jang'ombe walionekana kushambuliwa zaidi kipindi cha kwanza ingawa dakika ya 27 Yanga ililishambulia lango la wapinzani wao ingawa nao walifanikiwa kunusuru hatari hiyo langoni mwao na kumpa kazi nzito kipa wa Taifa Jang'ombe kuokoa mashambulizi yao.

Hii ndio mechi ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi huku kiungo mpya Abubakar Salum 'Sure Boy' akilishika vyema dimba la kati. Kwa upande wa kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery hakupata kashikashi nyingi kutoka kwa wapinzani wake kwani ngome yake ya ulinzi chini ya Nahodha Bakari Mwamnyeto ilionekana kuwa imara zaidi huku Deus Kaseke akiikosesha timu yake bao dakika ya 79 baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Taifa Jang'ombe hii ni mechi yao ya pili baada ya ile ya awali kufungwa na KMKM bao 2-1 ambapo Yanga itacheza mechi yao pili Ijumaa na KMKM.

Makocha wa timu hizo Cedric Kaze wa Yanga na Omar Khamis wa Taifa walifanya mabadiliko ya vikosi vyao ambapo Yanga alitolewa nje Dickson Ambundo/Crispin Ngushi ambaye amesajiliwa hivi karibuni akitokea Mbeya Kwanza pamoja na Nkane/Mapinduzi Balama Upande wa Taifa waliotoka ni Ahmed Mohamed/Khelef Saleh, Ali Makelele/Azak-rabin Mbarouk, Jamal Abdul/Joshua Salum, Yasir Masoud/Peter Stanley, Adil Nasor/Abdalla Mudhihir.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’