Baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji, kikosi cha Yanga kutakuwa na mapumziko ya siku tatu kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema baada ya kumaliza vyema mwaka 2021, wanahamishia nguvu zao kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo wao ni mabingwa watetezi
Mchezo wa kwanza wa Yanga kwenye michuano hiyo ni dhidi ya Taifa Jang’ombe ambao utapigwa uwanja wa Amaani, Januari 05
Yanga imepangwa kundi B pamoja na Taifa Jang’ombe na KMKM
ADVERTISE HERE