Mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ameondoka nchini kwenda kuungana na timu ya Taifa ya Mali kwa ajili ya kushiriki michuano ya AFCON 2021 inayoanza Januari 06 huko Cameroon
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa vinara hao wa ligi kuu wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinda lango wa Mtibwa Sugar Abdultwalib Mshery

Yawezekana leo Mshery ameitumikia Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union, akiibuka nyota wa mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani na Mtibwa kushinda bao 1-0
Mshery anatajwa kuwa pendekezo la benchi la ufundi kutokana na umahiri wake katika kudaka lakini pia matumizi ya miguu yake
ADVERTISE HERE