Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watakamilisha michakato ya usajili wa dirisha dogo kabla ya mwaka 2021 kumalizika
Mpaka sasa Yanga imetangaza usajili wa Salum Abubakar 'Sureboy' aliyetua kutoka Azam Fc akiwa mchezaji huru
Yanga imekuwa ikihusishwa na wachezaji kadhaa, Bumbuli amesema Wanayanga wasubiri taarifa kutoka kwa viongozi wao
"Uongozi unaendelea na michakato yake ya usajili, wakati mambo yakiwa tayari tutatoa taarifa. Tunatarajia wachezaji wapya tuwatumie kwenye kombe la Mapinduzi hivyo pengine mwishoni mwa wiki hii tutaweka hadharani kikosi kinachokwenda Zanzibar," alisema
Aidha, Mkuu huyo wa kitengo cha habari, amesema baada ya kuwatoa Ditram Nchimbi na Adeyum Saleh ambao mikataba yao imemalizika, hakuna mchezaji mwingine ambaye ataachwa akikanusha tetesi zilizokuwa zikiwahusisha kutolewa kwa mkopo Paulo Godfrey 'Boxer' na Abdallah Shaibu 'Ninja'
Nafasi ambazo zinatarajiwa kuongezewa nguvu ni pamoja na mlinda lango, mshambuliaji wa kigeni na kwenye safu ya ulinzi