Mabingwa hupita nyakati hizi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jan 2018
Mabingwa hupita nyakati hizi
Yanga imeendelea kusuasua kwenye ligi kuu ya Vodacom baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa tatu mfululizo leo dhidi ya Mwadui FC.

Kabla ya kuivaa Mwadui FC, katika mzunguuko wa 12 Yanga ililazwa mabao 2-0 na Mbao FC wakati pia ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons kwenye mzunguuko wa 11.

Matokeo haya ni dhahiri yanawaumiza mashabiki wa Yanga lakini hakuna namna zaidi ya kuyakubali kwani katika soka kuna wakati lazima yatokee.

Msimu huu Yanga imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na changamoto za nje ya uwanja. Aidha, majeruhi mfululizo kwa wachezaji wake muhimu ni pigo jingine.

Wachezaji wanaopata nafasi wamekuwa wakijituma kadiri ya uwezo wao, ni bahati mbaya tu matokeo hayapatikani.

Jambo hili hutokea. Muhimu ni kuendelea kuwaunga mkono bila shaka matokeo yatapatikana michezo ijayo.

Pia ikumbukwe Yanga ni mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa misimu mitatu mfululizo. Msimu wa 2014-15, 2015-16, na 2016-17 huku katika kipindi cha miaka 10, Yanga imetwaa mataji saba ya ligi!

Haya ni mafanikio ya kujivunia. Hakuna sababu ya kujihisi wanyonge na kurushiana lawama wakati timu inapokuwa haifanyi vizuri.

Matokeo haya yatumiwe na benchi la ufundi kusahihisha kasoro zinazo-onekana ili ushindi upatikane michezo ijayo.

Lazima mashabiki tufahamu kuna nyakati kama hizi zitatokea kwa Bingwa yeyote.

Kwa wale wanaofuatilia ligi za Ulaya sote tunafahamu timu kama Real Madrid inapita katika nyakati gani.

Kule Uingereza, Chelsea bingwa mtetezi, Manchester United, Arsenal nazo zinakumbana na hali hii kwa nyakati tofauti licha ya kuwa na vikosi imara.

Bingwa yeyote lazima atapita katika nyakati kama hizi.

Na uzuri historia inaonyesha Yanga haina rekodi ya kufanya vibaya kwa muda mrefu kama watani zetu waliokosa ubingwa kwa miaka mitano!

Kuchukua ubingwa mara saba katika kipindi cha miaka 10 inakuonyesha ni jinsi gani Yanga ina kawaida ya kujisahihisha kwa haraka zaidi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
58m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’