Baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Disemba 31 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Wananchi wataelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hii na wamepanga kurejesha taji hilo Jangwani kwa msimu wa pili mfululizo
Januari 05 watacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Taifa ya Jan'gombe na kukamilisha hatua ya makundi Januari 07 kwa mchezo dhidi ya KMKM
Yanga itawatumia nyota wake wapya watakaosajiliwa katika dirisha dogo pamoja na wachezaji ambao hawakutumika sana kwenye ligi
Michuano hii ni nafasi kwa kocha Nasreddine Nabi kujaribu wachezaji na mbinu mpya kabla ya kurejea kwa ngwe ya pili ya ligi na kombe la FA

ADVERTISE HERE