Mwanzoni mwa mwezi Januari 2022, michuano ya kombe la Mapinduzi inaanza visiwani Zanzibar, mabingwa watetezi Yanga wakitarajiwa kwenda kutetea ubingwa wao
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watakwenda Zanzibar kushiriki michuano hiyo wakiwa na kikosi chao kamili na zaidi Wananchi watarajie kuwashuhudia wachezaji wapya ambao watasajiliwa katika usajili wa dirisha dogo
Bumbuli amesema kabla ya Disemba 31, nyota wote waliosajiliwa watakuwa wamefahamika tayari kuelekea visiwani Zanzibar
Mpaka sasa Yanga inatajwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili, kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' ambaye jana alikabidhiwa barua ya kuvunja mkataba wake na Azam Fc
Pia Wananchi wanatajwa kumnasa winga kinda Denis Nkane kutoka Biashara United
Imeelezwa kuna usajili wa mlinda lango, mlinzi wa kati na mshambuliaji wa kigeni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Dominic Albinus ametamba kuwa siku sio nyingi nchi itatikisika pale utambulisho wa nyota wapya utakapofanyika..!