Tumedhamiria kushinda ubingwa - Saido

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Dec 2021
Tumedhamiria kushinda ubingwa - Saido

Kiungo wa Yanga, Saido Ntibazonkiza, amesema wanataendelea kupambana kuhakikisha wanatimiza lengo la kuwa mabingwa wa ligi kuu ya NBC msimu huu

Baada ya kuifunga Tanzania Prisons Jumapili, Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 23, ikifuatiwa na Simba yenye pointi 18.

Saido ambaye alisajiliwa Yanga wakati wa dirisha dogo msimu wa 2020/21, amesema wanaendelea kupambana ili kufanikisha azma ya kutwaa ubingwa na kasi waliyonayo sasa inawaaminisha hakuna cha kuwazuia.

"Bado mapambano yanaendelea na tutapambana kwa jasho kupata ushindi ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa"

"Mashabiki wanapenda kuona sisi tunashinda mechi zetu hili hata sisi tunalipenda pia, kwani ili kupata pointi tatu ni lazima kushinda pale ambapo tunacheza, tunaamini kwamba tutafanya vizuri," alisema Saido

Katika mabao 14 ambayo yamefungwa na Yanga kwenye michezo ya Ligi Kuu, Saido ametupia mabao mawili na ana pasi moja ya bao

Tangu arejeshwe kwenye kikosi cha kwanza baada ya Yacouba Songne kuumia, Saido amekuwa katika kiwango bora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’