Uongozi wa Azam Fc umeridhia kuvunja mkataba wa kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' baada ya mchezaji huyo kuwasilisha barua rasmi
Jana Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' alithitisha kuwa Sure Boy aliomba kuvunja mkataba wake na walimtaka aandike barua rasmi
Sure Boy alikuwa amebakisha mkataba wa miezi nane kuitumikia Azam Fc lakini klabu hiyo imeonyesha uungwana kwa kuvunja mkataba huo bila ya gharama yoyote
Azam Fc imetambua mchango wa Sure aliyeitumikia timu hiyo tangu mwaka 2008, na wamemtakia kila la kheri huko aendako
Sasa ni suala la muda tu, Sure Boy atatangazwa kuwa mchezaji wa Yanga ikielezwa amesaini mkataba wa miaka miwili
ADVERTISE HERE