Kocha Mkuu wa Yanga nasreddine Nabi amebainisha baadhi ya maeneo ambayo anahitaji kuyaboresha katika usajili wa dirisha dogo ambalo tayari liko wazi
Licha ya kujivunia ubora wa kikosi chake, Nabi amesema yapo maeneo ambayo yanahitaji kuimarishwa ili kutengeneza uwiano mzuri wa timu
Nabi amesema anahitaji mlinzi mmoja wa kati, mawinga wawili na mmoja kati yao awe anatumia mguu wa kushoto
Aidha, kocha huyo raia wa Tunisia amesema anahitaji kuiboresha safu ya ushambuliaji, akiomba kupatiwa mshambuliaji mzuri mmoja wa kati ili kuipa nguvu zaidi safu hiyo
"Tuna vijana wazuri kwenye timu yetu tena wenye moyo wa kujituma kwa ajili ya timu. Nawasifu sana kwa hilo lakini tunahitajika kujiimarisha zaidi kwa kuwa na uwiano nzuri kimbinu na kiufundi," alisema Nabi