Msimu uliopita Kibwana Shomari aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga
Alinza vyema msimu huu kabla ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Simba ambayo yanaweza kumuweka nje hadi wiki nne
Kwa mara ya kwanza Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo atapanga kikosi chake pasipo uwepo wa Kibwana aliyemuhamishia safu ya ulinzi wa kushoto baada ya ujio wa Djuma Shabani 'Soldier ya Bemba'
Katika nafasi ya Kibwana, Nabi anao wachezaji watatu David Bryson, Yassin Mustafa na Adeyum Saleh lakini bado alipendelea kumtumia Kibwana kutokana na uwezo wake mkubwa hasa katika kuzuia
Kukosekana kwake ni wazi kutamlazimisha Nabi kubadili mfumo, akitarajiwa kuanza na Bryson ambaye ameonyesha ubora pale timu inaposhambulia
Kibwana ameweka 'standard' upande wa kushoto, wenzake watahukumiwa kwa kufananisha ubora wao na vile Kibwana anacheza