Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu iko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa baadae leo katika uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga
Hafidh amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
"Kikosi kimewasili salama hapa Rukwa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Prisons. Wachezaji wako katika hali nzuri, tumepata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Nelson Mandela"
"Mpaka sasa hatua kesi yoyote mbaya kwa wachezaji tuliokuja nao ambayo inaweza kuwazuia wasicheze mchezo wa leo. Ni mchezaji mmoja (Yannick Bangala) tuliyemuacha Dar es salaam baada ya kukumbwa nachangamoto ya homa kali na mafua"
"Mashabiki wa Yanga na Watanzania wote watarajie burudani nzuri kutoka hapa Sumbawanga," alisema Hafidh