Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema baadhi ya wachezaji wake ni wagonjwa na hana uhakika kama wanaweza kutumika kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons hapo kesho
Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Nabi amesema bado hawezi kuthibitisha wachezaji wangapi wanaweza kukosekana kwenye mchezo huo kwa sababu itategemea na watakavyoamka
Aidha, Nabi ametoa salamu za pole kwa klabu ya Simba kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuumwa hivyo kushindwa kucheza mechi yao iliyopangwa kuchezwa leo dhidi ya Kagera Sugar
Nabi amesema afya ya mchezaji ni muhimu kuliko mchezo wenyewe hivyo anawaombea wachezaji wa Simba wapone haraka ili warudi kucheza.
ADVERTISE HERE