Simba, Yanga zaruhusiwa kutumia uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2018
Simba, Yanga zaruhusiwa kutumia uwanja wa Taifa
Timu za Simba na Yanga zimeruhusiwa kuanza kuutumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa baadhi ya mechi za ligi kuu Tanzania Bara na zile za kimataifa zilizo chini ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Simba ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuufungua uwanja huo katika mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Singida United utakaopigwa Alhamisi Januari 18 mwaka huu, huku Yanga wakiutumia Jumapili watakapokabiliana na Ruvu Shooting.

Mechi zote zitakuwa LIVE kupitia channel ya AzamSports2 ndani ya king'amuzi cha Azam TV.

Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema hatua hiyo imetokana na jitihada za bodi hiyo kuiomba serikali ambao ndiyo wamiliki wa uwanja huo, ambao wameziruhusu timu hizo kuutumia mara moja pekee kwa wiki.

Serikali iliufungia uwanja huo tangu mwezi Septemba mwaka jana kwaajili ya matengenezo ambayo tayari yamekamilika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’