Mabadiliko Yanga, taa ya kijani imewaka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Dec 2021
Mabadiliko Yanga, taa ya kijani imewaka

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Ofisi ya Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo Tanzania wamepitisha Katiba mpya ya mwaka 2021 ya Yanga ambayo iliridhiwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Juni 27, mwaka huu, Dar es Salaam.

Kukamilika kwa usajili wa Katiba hiyo, sasa kunaruhusu mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga kuendelea kama ambavyo imeanishwa katika mabadiliko ya katiba hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza amesema kukamilika kwa mchakato huo kunatoa fursa kwa yeye na timu yake kuanza kukamilisha mambo mbalimbali ambayo waliwaahidi wanachama wao kwenye mkutano mkuu ili kuona kwa vitendo mabadiliko waliyokusudia.

"Ni jambo zuri ambalo limemfurahisha kila mmoja wetu, unajua Yanga ni timu kubwa na haya mabadiliko tunayokwenda kuyafanya yataonesha namna mchezo wa soka ulivyo na faida siyo kwa Yanga tu, bali na taifa la Tanzania kwa ujumla."

"Kwahiyo tuipongeze serikali kwa kuridhia kupitisha mabadiliko haya nadhani sasa ni zamu ya mimi na timu yangu kuanza kutekeleza yale yote ambayo tumekusudia kuifanyia Yanga ikiwemo mabadiliko ya kiuendeshaji, miundombinu mizuri, usajili mzuri, lakini pia mafanikio ya ndani ya uwanja," alisema Senzo

Habari Leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’