Kikosi cha Yanga kinaondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea mkoani Rukwa tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili, Disemba 19 katika uwanja wa Nelson Mandela
Yanga inaondoka jijini Dar es salaam kwa usafiri kwa ndege hadi mkoani Mbeya ambako wataunganisha Sumbawanga
Ni msako wa alama tatu nyingine kwa Yanga ambayo inasaka ubingwa wa 28 ligi kuu
ADVERTISE HERE