Wachezaji wanne wa kikosi cha Yanga ni majeruhi, taarifa iliyotolewa na Yanga imebainisha
Kibwana Shomari, Yusufu Athumani, Fiston Mayele na Yacouba Songne wanaendelea kupatiwa matibabu
Wakati Mayele akiendelea vizuri, Yanga itawapeleka nje ya nchi Kibwana na Yusufu kwa ajili ya matibabu zaidi
Aidha Yanga imethibitisha kumrejesha Kocha Edna Lema kukinoa kikosi cha Yanga Princess
Katika hatua nyingine, Yanga itaweka hadharani wachezaji watakaosajiliwa na wale ambao wataongezewa mikataba na wengine ambao watatolewa kwa mkopo
Dirisha dogo la usajili limefuguliwa leo na litafungwa Januari 15 2022
ADVERTISE HERE