Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia mabadiliko ya Katiba ya Yanga yaliyofanywa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama mapema mwaka huu
Hatua hiyo ya Serikali inatoa nafasi kwa mchakato wa kuunda mfumo mpya wa Uendeshaji kuanza rasmi
Sasa Yanga inakwenda kwenye mfumo wa Uwekezaji ambapo Wanachama watabaki na hisa asilimia 51 huku asilimia 49 zikienda kwa wawekezaji
Ili kuepuka sintofahamu kama iliyotokea kwa watani zao Simba wakati wanabadili mfumo wao, Yanga imeishirikisha Serikali hatua kwa hatua ili kuhakikisha mchakato wake unafanyika kwa mujibu wa matakwa ya Sheria

ADVERTISE HERE