Yanga kucheza uwanja wa Uhuru leo, Simba uwanja wa Taifa kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2018
Yanga kucheza uwanja wa Uhuru leo, Simba uwanja wa Taifa kesho
Jana wakati anazungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alizungumzia viashiria vya klabu ya Simba kubebwa baada ya Yanga kunyimwa ruhusa ya kutumia uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC huku Simba ikiruhusiwa kutumia uwanja huo kwenye mchezo wao dhidi ya Singida United kesho.

Hili ni tukio la pili kwani hata Yanga ilipocheza dhidi ya Prisons ilihamishiwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi huku Simba ikitumia uwanja wa Taifa kesho yake.

Kimsingi kuna matukio mengi ya kutia shaka Yanga imekuwa ikifanyiwa msimu huu.

"Tunatambua kwamba uwanja wa Taifa ulikuwa katika matengenezo na haujatumika kwa muda mrefu lakini kwa sasa unaonekana umekamilika, tulijaribu kuomba tuweze kuutumia lakini tumekosa hiyo fursa na tumepata taarifa kwamba kuna baadhi ya mechi zitachezwa pale lakini sisi mechi yetu ya kesho (Jumatano) itachezwa uwanja wa Uhuru," alisema Mkwasa.

"Tulitegemea tungeanza kucheza pale lakini tunakosa hiyo fursa sasa inatupa shida upande wetu tunaonekana kama hatupewi thamani au umuhimu."

"Nakumbuka mechi yetu na Prisons Yanga ilicheza Jumamosi, Simba wakacheza Jumapili lakini sisi tukacheza kwenye uwanja wa Azam Complex Simba wakacheza uwanja wa Uhuru kwa hiyo sisi tukakosa hiyo fursa, hii ni mara ya pili inakuwa wenzetu wanaanza kucheza na Singida Alhamisi kwenye uwanja wa taifa sisi kesho tumeambiwa tunacheza uwanja wa Uhuru."

"Sasa angalieni namna gani hakuna usawa katika mambo kama haya, sisi tunaomba kuwepo na usawa kwa sababu hizi timu zote ni za watanzania wazalendo, kama kuna haki basi itolewe kwa sawa kwa vilabu vyote kuliko kubagua kwamba timu hii inatumia uwanja fulani hii inakosa fursa."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’