Baada ya mchezo dhidi ya Simba uliopigwa juzi na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumatano, Disemba 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Benchi la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi linauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa hasa kutokana na malengo ya Yanga msimu huu ni kushinda mataji yote ya ndani
Ihefu Fc watarajie kukutana na 'mziki' uleule uliwatoa jasho Simba juzi na kupelekea mashabiki wa Simba wafanye sherehe baada ya kufanikiwa kupata sare
ADVERTISE HERE