Uongozi wa klabu ya Yanga umelaani kauli iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Wanachama klabu ya Simba Murtaza Mangungu baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kupitia vyombo vya Habari, Mangungu aliishutumu Yanga kuwa kuna viongozi wake waliingia VVIP pasipo kuwa na tiketi wala kadi huku Mtendaji Mkuu wa Simba akizuiwa kuingia
Aidha, Yanga imeitaka TFF kufanya uchunguzi wa kauli iliyotolewa na Mangungu kuwa Shirikisho hilo limepanga kuipa Yanga ubingwa
Yanga imetaka uthibitisho wa kauli hiyo na kuitaka TFF kuchukua hatua kwani lengo la kauli hiyo ni kutaka kuiaminisha jamii kuwa kuna mpango wa kupanga matokeo baina ya TFF na Yanga
ADVERTISE HERE